Dodoma FM
Dodoma FM
20 January 2026, 3:47 pm

Ziara hiyo imewahusisha viongozi wa kanda namba 3 pamoja na viongozi mbalimbali za serikali kutoka kata ya Zuzu.
Na Lilian Leopold.
Viongozi wa kanda namba tatu wafanya ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya elimu inayotekelezwa katika shule ya sekondari Zuzu jijini Dodoma, kwa lengo la kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.
Ziara hiyo imewahusisha viongozi wa kanda namba 3 pamoja na viongozi mbalimbali za serikali kutoka kata ya Zuzu, ambapo walipata nafasi ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mchumi wa kanda namba tatu, Vestina Manota, amesema serikali imeendelea kuboresha na kuwekeza katika miradi ya elimu ili kuweka mazingira rafiki na bora kwa ajili ya wanafunzi na walimu.