Dodoma FM

Muda wa uandikishaji uchaguzi Machinga waongezwa

15 January 2026, 11:02 am

Picha ni Meneja wa soko la wazi la Machinga Complex, CPA Johnstone Kahungu akizungumza na waandishi wa habari katika soko hilo. Picha na Lilian Leopold.

Zoezi la uchaguzi wa viongozi wa soko la wazi la Machinga Complex linatarajia kufanyika Januari 24, 2026 ambapo wafanyabiashara watapigia kura viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi, Katibu Mkuu ,Katibu Msaidizi, Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa makundi maalum.

Na Lilian Leopold.

Zoezi la uandikishaji kuelekea uchaguzi wa viongozi wa soko la wazi la Machinga Compex jijini Dodoma limeingia hatua mpya baada ya mamlaka inayosimamia uchaguzi huo kuongeza muda wa kujiandikisha kwa siku mbili kuanzia tarehe 14 hadi 15, 2026. Hatua inayolenga kuwapa fursa wafanyabiashara ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha awali.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, baada ya kupokea malalamikokutoka kwa wafanyabiashara alipotembelea soko hilo tarehe 08 Septemba 2025, wakilalamikia mwenendo wa uongozi uliopo na kuhitaji mabadiliko.

Akizungumza na waandishi wa habari katika soko hilo, Menejawa Soko la wazi la Machinga Complex, CPA Johnstone Kahungu amesema kuwa uamzi wa kuongeza umetokana na wafanyabiashara wengi kutokujiandikisha hapo awali.

Sauti ya Johnstone Kahungu.
Picha ni baadhi ya wafanyabiashara waliojitokeza katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa soko la wazi la Machinga Compex jijini Dodoma. Picha na Lilian Leopold.

Kwa upande wao, baadhi wafanyabishara wameeleza kufurahishwa na uamzi huo, huku wakiwataka wafanyabiashara wenzao kujitokeza kwa wingi na kuchagua viongozi wanaowajibika.

Sauti za wafanyabiashara.