Dodoma FM

Mbwa wanaozagaa mitaani Dodoma wageuka tishio kwa wananchi

7 January 2026, 2:25 pm

Wananchi wameuomba uongozi wa serikali za mitaa kushughulikia tatizo la mbwa mtaani kwani ni tishio hususan kwa watoto. Picha na Mtandao.

Malalamiko haya yanakuja baada ya wananchi kudai kuwa tayari walishawasilisha tatizo hilo kwa uongozi wa serikali za mitaa, lakini hadi sasa hakuna jitihada zozote zilizofanyika kudhibiti mbwa hao.

Na Lilian Leopold.

Wananchi wa mtaa wa Miyuji Proper, kata ya Miyuji  jijini Dodoma wamelalamika tatizo la mbwa kuzagaa  mtaani hovyo , hali inayohatarisha usalama wa watoto na wananchi kwa ujumla hususani katika kipindi ambacho wanafunzi wanakaribia kufungua shule.

Taswira ya habari imefika mtaani hapo na kuzungumza na baadhi ya wananchi, ambapo wamesema tatizo la mbwa kuzagaa mtaani limekuwepo kwa muda mrefu jambo linalo walazimuu wazazi kutumia muda mwingi kuwasindikiza watoto wao kwenda na kurudi shule kwa kuhofia watadhuriwa na mbwa hao.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Balozi wa shina namba 13, mtaa wa Miyuji Proper Dickson Lazaro amekiri kuwepo wa tatizo la mbwa kuzagaa mtaani kwa kipindi kirefu, huku akibainisha hatua alizozichukua kuhakikisha wananchi wanakua salama.

Sauti ya Dickson Lazaro.

Akijibu malalamiko hayo, Diwani wa kata ya Miyuji Ringo Iringo amesema tayari amelipokea suala hilo na hatua za kulifanyia kazi zinaendelea, huku akiwaomba wananchi kuwa wavumilivu wakati taratibu za kudhibiti mbwa hao zikiendelea.

Sauti ya Ringo Iringo.

Sambamba na hilo Diwani Ringo ametoa wito kwa wamiliki wa mbwa kuwajibika ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwafunga, kuwachanja na kuwatunza mbwa wao, ili kuepusha  madhara yanayoweza kujitokeza kwa wananchi kutokana na mbwa kuzagaa mtaani.

Sauti ya Ringo Iringo.