Dodoma FM
Dodoma FM
16 December 2025, 5:23 pm

mikakati na miongozo iliyowekwa serikali pia imechagiza watu wenye ulemavu kushiriki katika mikutano ya ngazi za maamuzi.
Na Yussuph Hassan.
Imeelezwa kuwa kumekuwa na mwamko mkubwa kwa watu wenye ulemavu kushiriki katika kutoa mawazo yao katika mikutano ya kijamii katika ngazi ya maamuzi.
Hayo yamebainishwa na afisa ustawi wa jamii Mwandamizi Oliver kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wakati akizungumza na kituo hiki.
Bi Oliver amesema kwa sasa ushiriki wa watu wenye ulemavu ni mkubwa ambapo hamasa hii pia imechangia na kuwepo kwa viongozi mbalimbali wanaowakilisha kundi hilo.
Aidha amesema mikakati na miongozo iliyowekwa serikali pia imechagiza watu wenye ulemavu kushiriki katika mikutano ya ngazi za maamuzi.