Dodoma FM

Ukosefu wa elimu changamoto kwa makundi kupata mkopo wa 10%

12 December 2025, 4:33 pm

Kukosa mikopo ya 10% kunapelekea makundi hayo kujiingiza katika mikopo umiza .Picha na Mtandao.

wamesema kuwa endapo watapata mikopo ya asilimia kumi itawasaidia kukuza uchumi wa biashara zao kutoana na wanawae hao kuwa na mitaji midogo.

Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa ukosefu wa elimu kwa makundi ya wanawake na vijana ni moja ya changamoto inayokwamisha makundi hayo kupata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa kutokana na mapato ya halmashauri.

Baadhi ya wakina mama wa kijiji cha Mpwayungu wamesema kuwa kukosa fursa ya mikopo ya asilimia kumi imepelekea kujiingiza katika mikopo holela inayowaumiza kutokana na riba kuwa kubwa.
Hivyo wamesema kuwa endapo watapata mikopo ya asilimia kumi itawasaidia kukuza uchumi wa biashara zao kutoana na wanawae hao kuwa na mitaji midogo.

Kutokana na mitaji midogo waliyonayo wanawake hao wamesema endapo watapata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri itawasaidia kukuza uchumi wao na kuepukana na mikopo ya riba kubwa.

Sauti za wanawake.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji Mpwayungu bw.Festo Manjechi amesema wananchi wamejitahidi kuunda vikundi kwa ajili ya kupata mikopo lakini mpaka sasa hakuna mafanikio ya kupata fedha hizo za halmashauri.

Sauti ya bw.Festo Manjechi.

Manjechi ameongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwavunja moyo vijana hao pamoja na akinamama kwani baadhi ya wachache wamekuwa wakinufaika na mikopo kutoka bank ya vision Fund iliyopo chini ya shirika la Innovation of Africa.

Sauti ya bw.Festo Manjechi.

Taswira ya habari imefanya jitihada ya kumtafuta Ndg.Stephano Sholla ambaye ni Afisa Maendeleo katika kijiji Cha Mpwayungu lakini haikuweza kumpata kutoka na mjukumu mengine ya kiserikali.
Ikumbukwe kuwa mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri imelenga kuinua uchumi wa vijana, wanawake na makundi maalum ambapo wanawake hupewa 04%, vijana 04% na watu wenye ulemavu 02%.