Dodoma FM

TASAF yaboresha maisha ya wakazi wa Igandu

11 December 2025, 4:53 pm

Kupitia TASAF wamefanikiwa kuboresha makazi yao na hata kujimu.Picha na mtandao.

Tofauti na hapo awali ambapo baadhi ya watoto walikaa majumbani Kwa kukosa uwezo wa kumudu kununua viafaa vya shule.

Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kijiji Cha Igandu Wilaya ya Chamwino wameipongeza Serikali kupitia mfuko wa TASAF Kwa kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wasio jiweza kijijini hapo.

Wakizungumza baadhi ya wanufaika wamesema kuwa kupitia TASAF wamefanikiwa kuboresha makazi yao na hata kujimu kuendesha biashara sambamba na kupeleka watoto mashuleni.

Sauti za wanufaika.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bi.Joyce Chiloweka amekiri mfuko huo wa kusaidia Kata masikini umekuwa mkombozi Kwa wananchi wake.

Chiloweka amesema kuwa Baadhi ya familia hazikuwa na uwezo wa kusomesha na hata kujikimu katika mahitaji yao ya chakula lakini kupitia mfuko wa TASAF ziliweza kubadilisha mfumo wa maisha.

Sauti ya Bi.Joyce Chiloweka