Dodoma FM

Machinga Complex yaendelea na shughuli, ulinzi waimarishwa

10 December 2025, 3:36 pm

Picha ni soko la wazi la Machinga Complex jijini Dodoma. Picha na Dodoma FM.

Hali ya ulinzi na usalama imeendelea kuimarishwa na vyombo vya usalama, huku wafanyabiashara wakijitokeza na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Na Lilian Leopold.

Wafanyabiashara wa soko la wazi la Machinga Complex jijini Dodoma wameendelea kurejea katika shughuli zao za kila siku, baada ya kutumia siku ya tarehe 09 Desemba kupumzika majumbani kama ilivyoelekezwa na serikali.

Hatua hii imekuja kufuatia tamko la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambalo alilitoa wakati akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa wananchi akiwatakia heri ya siku ya Uhuru inayoadhimishwa tarehe 09 Desemba kila mwaka,Waziri Mkuu aliwasihi wananchi wote waliokuwa hawana dharura za kikazi kuitumia siku hiyo kwa mapumziko majumbani.

Katika kufuatilia hali baada ya siku hiyo, Taswira ya Habari imezungumza na Mbwana Hassan Kasonta, Afisa Biashara wa soko la wazi la Machinga Complex, ili kufahamu mwenendo wa biashara pamoja na hali ya ulinzi na usalama sokoni hapo.

Sauti ya mahojiano na Mbwana Hassan Kasonta.