Dodoma FM
Dodoma FM
4 December 2025, 11:47 am

Kongamano hilo limeelezwa kuwa muhimu katika kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu haki na ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye maamuzi ya kiuchumi.
Na Farashuu Abdallah.
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imetenga zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuwezesha makundi maalumu kushiriki kwenye miradi ya kiuchumi.
Sheria ya Ununuzi wa Umma imeelekeza taasisi zote za umma kutenga asilimia 30 ya manunuzi yote kwa ajili ya makundi maalumu wakiwemo vijana ili kuongeza ushiriki wao katika uchumi wa Taifa, kukuza ujasiriamali na kupunguza ukosefu wa ajira.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika chuo cha Mipango kwenye kongamano la umuhimu wa ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye fursa za kiuchumi Mkoani Dodoma, Meneja Uhusiano wa PPRA Remija Salvatory amesema fedha hizo zinalenga kuongeza ushiriki wa makundi hayo kwenye fursa za ununuzi wa umma.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Shivyawata mkoa wa Dodoma Mwalimu Omary Lubuva amesema pamoja na juhudi za Serikali watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto za uelewa mdogo wa namna ya kutumia fursa hizo na kukosa taarifa za zabuni.