Dodoma FM

Wananchi Ihumwa waipongeza NIDA kwa kusogeza huduma karibu

1 December 2025, 4:54 pm

Wamesema kuwa hivyo watatumia fursa hiyo kuhakikisha wanapata vitambulisho.Picha na Nida.

Kupitia taarifa ya 2024, NIDA imejisajili na kutambua jumla ya watu miloni 24.5 tangu kuanzishwa kwa zoezi (2012). Kutoka idadi hiyo, NIDA imetoa Namba za Utambulisho (NIN) kwa watu milioni 20.8

Na Victor Chigwada.
Wananchi wa mitaa ya Ihumwa,Chilwana na Chang’ombe kata ya Ihumwa wameiopengeza serikali kupitia mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kuwasogezea huduma karibu.

Hayo yanajiri baada ya ya mamlaka hiyo kutia kambi ya kufanya usijali wa kupata vitambulisho vya Taifa katika kata hiyo leo hii.

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa vitambulisho vya taifa ni muhimu kutokana na kuhitajika katika kuomba nafasi za kazi na katika biashara, hivyo watatumia fursa hiyo kuhakikisha wanapata vitambulisho.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Ihumwa Lamecki Mbinda amewasisitiza wananchi wa eneo lake kujitokeza kwa wingi ili kufanikiwa kuwa na utambulisho wa taifa.

Sauti ya mwenyekiti.