Dodoma FM
Dodoma FM
27 November 2025, 2:04 pm

Pamoja na hayo Wananchi wa Chamwino wamesisitiza kuwa elimu ya kitaalamu kuhusu namna ya kukabiliana na tembo itasaidia kupunguza madhara na kuimarisha usalama wa jamii pamoja na mazao yao.
Wananchi wa vijiji vya Chinugulu na Manda, tarafa ya Mpwayungu, Wilaya ya Chamwino, wameiomba Serikali kupeleka elimu ya namna ya kuwazuia tembo wasivamie mashamba yao, badala ya kutumia njia za kienyeji ambazo hazijawa suluhu ya tatizo hilo.
Wananchi hao wamesema njia za jadi wanazozitumia, ikiwemo kupuliza mavuvuzela, kengele na kufanya makelele, hazijasaidia kuzuia tembo, na mara kadhaa zimepelekea mazao na makazi kuharibiwa pamoja na baadhi ya wananchi kujeruhiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Sanjeli Charura amesema changamoto hiyo imekuwa ikijirudia kila msimu wa kilimo na mavuno, na kusababisha hofu kubwa kwa wakulima ambao hutegemea mazao yao kwa chakula na kipato.