Dodoma FM
Dodoma FM
26 November 2025, 3:33 pm

Kuwa kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania na ni msingi muhimu wa kuendeleza umoja.
Na Anwary Shaban.
Wananchi katika Jiji la Dodoma na Watanzania kwa ujumla wamehamasishwa kuendelea kulinda na kudumisha amani ya nchi muda wote.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemery Senyamule, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jukumu la jamii katika kuimarisha utulivu na mshikamano wa kitaifa.
Kwa upande wao, viongozi wa dini wamesisitiza kuwa kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania na ni msingi muhimu wa kuendeleza umoja pamoja na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi nchini.