Dodoma FM
Dodoma FM
13 November 2025, 4:48 pm

Kukamilika kwa bwawa hilo itawasaidia wananchi kufanya kilimo cha mwaka mzima tofauti na hapo awali ambapo kilimo kilitegemea msimu mmoja wa mvua.
Na Victor Chigwada.
Licha ya ujenzi wa bwawa la umwagiliaji kata ya Membe, wilaya ya Chamwino jijini Dodoma kusuasua lakini bado yapo matumaini ya kukamilika kwa mradi huo na kuanza kutumika katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji.
Hayo yameelezwa na Msimamizi wa ujenzi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji NIR Eng.Salehe Ahamadi ambapo amesema kuwa wameanza kupanga mikakati ya kuhakikisha wakulima wanaanza kutumia bwawa hilo.
Ahamadi ameongeza kuwa ni vyema wananchi kuwa na utayari wa kilimo Cha umwagiliaji kwani malengo ya ujenzi wa bwawa hilo yanaenda kutimia muda wowote.
Eng. Ahamadi amesisitiza kuwa ni muhimu wananchi kuwa tayari kwa kilimo cha umwagiliaji kwani malengo ya ujenzi wa bwawa hilo yanaendelea kutimia.
Nao baadhi ya wakazi wa Membe wameipongeza serikali kwa azma yake ya kuwasaidia wakulima kupitia kilimo cha umwagiliaji, wakisema bwawa hilo litawasaidia kufanya kilimo cha mwaka mzima tofauti na hapo awali ambapo kilimo kilitegemea msimu mmoja wa mvua.