Dodoma FM
Dodoma FM
10 November 2025, 1:20 pm

Awali, nilikutana na Fanikiwa na kukuandalia taarifa hii fupi, ikieleza jinsi mdogo wake alivyomsaidia kuachana na matumizi hayo na kuanza upya maisha yenye matumaini.
Na Seleman Kodima.
Fanikiwa Subukheri—sio Jina lake halisi —ni kijana mdogo aliyewahi kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya aina ya skanka, lakini hatimaye alifanikiwa kuchomoka katika janga hilo kwa msaada wa mdogo wake.
Hatua hiyo inakuja wakati ambapo ripoti ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya—DCEA—imebainisha ongezeko la wanawake wengi kununua na kutumia skanka, aina ya bangi yenye kemikali kali zaidi.
Kwa mujibu wa DCEA, skanka husindikwa hadi kufikia kiwango cha kemikali cha asilimia 40, tofauti na bangi ya kawaida yenye asilimia 8 hadi 15, hali inayosababisha madhara makubwa kwa afya ya akili na mwili.