Dodoma FM
Dodoma FM
28 October 2025, 3:05 pm

Jeshi la Polisi limewataka wananchi, vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kushirikiaa na vyombo vya usalama ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa amani, utulivu na uwazi.
Na Anwary Shaban.
Jeshi la Polisi mkoani limetoa tamko kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, likisisitiza kuwa limejipanga kuhakikisha amani na usalama vinatawala katika kipindi chote cha uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime, amesema wananchi wanapaswa kutumia haki zao za kikatiba kwa kwenda kupiga kura kwa amani bila kuingiwa na hofu.
Aidha, jeshi hilo limeonya kuwa halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani au uchochezi wa vurugu kwa kisingizio chochote.