Dodoma FM
Dodoma FM
27 October 2025, 3:20 pm

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Uchaguzi (NEC), uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 29, 2025, ambapo wananchi kote nchini watapata nafasi ya kuchagua viongozi wao katika ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani.
Na Lilian Leopold.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Alhaj Jabir Shekimweri, amewahakikishia wananchi kuwa maandalizi yote ya kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025 yamekamilika kwa asilimia 100.
Akizungumza na waandishi wa habari, Shekimweri amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo tayari kuhakikisha kila raia mwenye sifa na haki ya kuchagua kiongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani anapata haki yake ya kupiga kura kwa amani na utulivu.
Ameongeza kuwa mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu, wazee, na wakina mama wajawazito yameimarishwa, na usalama wao umehakikishwa kikamilifu.