Dodoma FM
Dodoma FM
24 October 2025, 3:00 pm

Mitandao ya kijamii wameweza imewezesha kujifunza mambo mbalimbali, kupata taarifa na kufanya biashara kupitia mitandaoni.
Na Anwary Shaban.
Wananchi wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kama fursa ya kukuza uchumi, kuongeza maarifa, na kuboresha shughuli zao za kila siku badala ya kuitumia kwa mambo yasiyo na tija.
Wito huo umetolewa na Pascal Mosses Mwakanyamale, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Geovate Company, iliyopo jijini Dodoma wakati akizungumza na Taswira ya Habari amesema mitandao ya kijamii imekuwa nyenzo muhimu katika ulimwengu wa sasa, hasa katika kukuza biashara ndogondogo, utafutaji wa taarifa, na kujifunza mambo mapya.
Nao baadhi ya wananchi wamesema kupitia mitandao ya kijamii wameweza kujifunza mambo mbalimbali, kupata taarifa na kufanya biashara kupitia mitandaoni.
Aidha, Pascal Mosses ameikumbusha jamii kutumia akili mnemba (maarufu kama Artificial Intelligence – AI) kwa matumizi sahihi, ikiwemo katika kujifunzia mambo mapya na kubuni suluhisho za kiteknolojia zitakazochochea maendeleo.