Dodoma FM

Matumizi ya mtandao yazingatiwe kuongeza ubunifu

9 October 2025, 12:32 pm

Matumizi sahihi ya mtandao yanachangia kukuza ubunifu na maarifa katika nyanja mbalimbali. Kupitia teknolojia hii, watu wanaweza kupata taarifa, kujifunza mbinu mpya, na kubuni mawazo yatakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Picha na Google.

Bi. Lawi ameongeza kuwa mtu anaweza kuunganishwa na mtandao kwa kutumia modemu, Wi-Fi za majumbani na ofisini, au huduma za intaneti zinazotolewa na kampuni za simu, ambazo zimekuwa kiunganishi muhimu katika ulimwengu wa kidijitali.

Na Anwary Shaban.

Jamii imetakiwa kutumia mtandao kwa njia sahihi ili kuongeza maarifa, kuboresha mawasiliano, na kuongeza tija katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza na Taswira ya Habari Bi. Lusina Lawi kutoka Kitengo cha Kompyuta, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la Dodoma, amesema matumizi bora ya mtandao yana mchango mkubwa katika kusaidia watu kupata taarifa kwa haraka na kujifunza kupitia njia za kidijitali.

Sauti ya Lusina Lawi.

Bi. Lawi ameongeza kuwa mtu anaweza kuunganishwa na mtandao kwa kutumia modemu, Wi-Fi za majumbani na ofisini, au huduma za intaneti zinazotolewa na kampuni za simu, ambazo zimekuwa kiunganishi muhimu katika ulimwengu wa kidijitali.

Sauti ya Lusina Lawi.

Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Kompyuta cha Dar es Salaam (UCC) wamesema mtandao ni sehemu muhimu ya maisha yao ya kila siku, hususan katika masuala ya kitaaluma na kijamii, kwani huwasaidia kufanya utafiti, mawasiliano na kujifunza kwa urahisi.

Sauti za wanafunzi.

Kutokana na umuhimu wa teknolojia ya mawasiliano, jamii imeshauriwa kuendelea kuelimishwa kuhusu matumizi salama na yenye tija ya mtandao, ili kuepuka changamoto kama uhalifu wa mtandaoni, upotoshaji wa taarifa, na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.