Dodoma FM
Dodoma FM
8 October 2025, 11:54 am

Wameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yanayosifika kwa utulivu na amani, hivyo ni jukumu la kila mmoja kulinda tunu hiyo muhimu kwa kushiriki uchaguzi kwa utulivu na bila viashiria vya vurugu.
Na Victor Chigwada.
Licha ya mijadala mbalimbali kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu, wananchi wameendelea kuhamasishana kudumisha amani sambamba na kujitokeza kupiga kura kwa wingi.
Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wananchi wa Chinangali, Wilaya ya Chamwino, ambao wamesisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.
Aidha, wamewataka vijana kuachana na taarifa potofu zinazozagaa mitandaoni zinazohamasisha maandamano na vitendo vya uvunjifu wa amani, badala yake wajikite katika kushiriki kikamilifu mchakato wa demokrasia kwa njia za kisheria.
Wameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yanayosifika kwa utulivu na amani, hivyo ni jukumu la kila mmoja kulinda tunu hiyo muhimu kwa kushiriki uchaguzi kwa utulivu na bila viashiria vya vurugu.
Serikali ya Tanzania imeweka msisitizo mkubwa kuhusu ushiriki wa vijana katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ikitambua kuwa vijana ni nguvu muhimu katika kuleta mabadiliko chanya na maendeleo ya taifa.