Dodoma FM

Watumishi wa umma watakiwa kuzingatia maadili kazini

3 October 2025, 10:51 am

Picha ya pamoja ya watumishi wa umma na Naibu Katibu Mkuu Bi. Hilda Kabissa alipokuwa akifungua kikao kazi cha sita cha wadau wa usimamizi wa maadili ya kitaaluma na utendaji. Picha na Selemani Kodima.

Hili linajiri baada ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupokea malalamiko ya wananchi juu ya baadhi ya watumishi wa umma kutumia lugha zisizofaa,kutojali utu na kutoa majibu yanayokatisha tamaa wateja.

Na Selemani Kodima.

Watumishi wa umma nchini wametakiwa kuzingatia Sheria,taratibu na mienendo ya maadili ya utendaji wa taaluma zao wakiwa kazini ili kuboresha hali ya utoaji wa huduma kwa kuzingatia Weledi,uadilifu na uwajibakiji wa hiari.

Hili linajiri baada ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupokea malalamiko ya wananchi juu ya baadhi ya watumishi wa umma kutumia lugha zisizofaa,kutojali utu na kutoa majibu yanayokatisha tamaa wateja.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Bi. Hilda Kabissa ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, alipokuwa akifungua kikao kazi cha sita cha wadau wa usimamizi wa maadili ya kitaaluma na utendaji kilichofanyika Oktoba 2, 2025, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, jijini Dodoma.

Sauti ya Bi. Hilda Kabissa.

Aidha ametoa agizo kwa waajiri wote wa utumishi wa umma nchini kuweka kipaumbele katika utoaji wa mafunzo ya maadili kwa watumishi wapya na walioko kazini.

Sauti ya Bi. Hilda Kabissa.

Kwa upande Mwingine ,Bi Hilda amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma, jambo lililochangia nchi kupanda kutoka nafasi ya 87 mwaka 2023 hadi nafasi ya 82 mwaka 2024 katika tathmini ya Shirika la Transparency International.

Awali Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili, Bi. Felister Shuli, amesema kuwa kikao kazi hicho ni matokeo ya maazimio ya kikao cha tatu kilichofanyika Septemba 2023 jijini Dodoma, ambapo iliazimiwa vikao kama hivyo vifanyike mara mbili kwa mwaka kwa mfumo wa mzunguko.

Akitoa Shukrani na Ahadi juu ya Utekelezaji wa Maagizo hayo,Mwenyekiti wa kikao, Bw. Salvatory Kilasara kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, amesema watahakikisha hatua zote na maelekezo yote yaliyotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wanayatekeleza ipasavyo.