Dodoma FM
Dodoma FM
5 September 2025, 5:40 pm

Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973 na marekebisho yake, kila dereva wa chombo cha moto anatakiwa kuendesha kwa kasi isiyozidi viwango vilivyowekwa, kuzingatia alama na michoro ya barabarani, pamoja na kuhakikisha usalama wa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kata ya Ihumwa jijini Dodoma wameeleza hofu yao juu ya ongezeko la matumizi ya vyombo vya moto, ikiwemo bodaboda, magari ya kampuni za mizigo na magari ya kubeba vifusi, wakisema madereva wengi wamekuwa wakiendesha kwa mwendo kasi na kuhatarisha usalama wa wananchi.
Baadhi ya wananchi wamesema hali hiyo inawaweka kwenye hatari kubwa hasa watoto na wazee wanaotembea kwa miguu barabarani.
Kwa upande wake, Inspector Kutega, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kata ya Ihumwa, amesema tayari upo utaratibu wa kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto kabla ya kuchukua hatua kali za kisheria.
Ameongeza kuwa, hivi karibuni jeshi hilo litaandaa semina maalum kwa vijana wa Ihumwa ili kuhakikisha usalama barabarani unadumishwa.