Dodoma FM
Dodoma FM
3 September 2025, 5:50 pm

Na Yussuph Hassan.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Mongosso Wambura, amesisitiza kuwa usalama wa waandishi wa habari ni suala la kipaumbele kwa Jeshi la Polisi, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
IGP Wambura ametoa kauli hiyo jijini Dodoma katika kongamano la amani lililowakutanisha waandishi wa habari na Jeshi la Polisi, likiwa na lengo la kujadili namna bora ya kudumisha amani na usalama katika kipindi cha uchaguzi.
Akizungumza kwenye mkutano huo, IGP Wambura alisema kuwa waandishi wa habari wanatekeleza jukumu nyeti katika taifa, hivyo ni wajibu wa jamii nzima kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira salama.