Dodoma FM

Jeshi la Polisi latoa ufafanuzi matukio ya utekaji

2 September 2025, 4:43 pm

Picha ni Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime akiongea na waandishi wa habari.Picha na Jeshi la Polisi.

Na Yussuph Hassan.
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa ufafanuzi kuhusu matukio ya utekaji na kupotea kwa watu ambayo yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara katika vituo vya polisi ambapo kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa kwa kina, imebainika kuwa si matukio yote yanayotokana na uhalifu wa kweli, bali mengine yamekuwa yakisababishwa na sababu binafsi au za kijamii

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, amesema kuwa baadhi ya matukio hayo yanatokana na watu kujiteka wenyewe, wivu wa mapenzi, imani za kishirikina, migogoro ya kugombea mali, pamoja na nia ya kulipiza kisasi.

Sauti ya (DCP) David Misime.