Dodoma FM
Dodoma FM
28 August 2025, 3:59 pm

Mwabukusi ameeleza kuwa mazungumzo hayo na Rais yatazingatia kutoa ushauri wa hatua za haraka kuchukuliwa ili kurudisha imani ya wananchi na kuhakikisha uchaguzi unakuwa shirikishi, shindani na wenye uhalali wa kisiasa.
Na Yussuph Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 27 Agosti, 2025.
Itakumbkwa kuwa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS kiliomba kukutana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dharura ili kuweza kuwasilisha kwake naoni ya wadau mbalimbali juu ya changamoto ambazo zinapaswa kutatuliwa kabla ya uchaguzi ili kuliwezesha taifa kuingia kwenye uchaguzi likiwa na amani na haki iweze kutendeka katika uchaguzi huo.