Dodoma FM

Jeshi la Polisi Tanzania mguu sawa kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu 2025.

28 August 2025, 3:33 pm

Picha ni Msemaji wa Jeshi la polisi DCP David Misime.Picha na Jeshi la Polisi.

Vilevile, limewakumbusha wagombea kuzingatia ratiba na muda wa kampeni uliopangwa ili kuepuka mivutano, migongano au migogoro itakayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Na Mariam Kasawa.
Jeshi la Polisi Tanzania limesema lipo tayari kuhakikisha amani, utulivu na usalama vinaendelea kudumishwa wakati wote wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, zilizo anza rasmi leo, Agosti 28, kama ilivyotangazwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Kupitia taarifa iliyotolewa Agosti 27, 2025 na Msemaji wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, DCP David Misime, Polisi imesisitiza kuwa imejiandaa ipasavyo kulinda mchakato wa kampeni za wagombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika maeneo yote ya nchi.

Aidha, Polisi imewaasa wagombea, wafuasi wao na wananchi kwa ujumla kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa kitaifa, huku ikisisitiza kwamba jukumu la kudumisha utulivu ni la Watanzania wote.

Sauti ya DCP David Misime.