Dodoma FM

Dawati kuwachukulia hatua wazazi wanao toa adhabu za vipigo vikali

28 August 2025, 3:13 pm

Je, ni sababu gani hasa huwafanya wazazi au walezi kutumia adhabu ya vipigo vikali kwa watoto.Chanzo na EATV.

Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inasimama kidete kupinga vipigo vikali na ukatili wa aina yoyote dhidi ya watoto. Inasisitiza malezi yenye upendo, heshima na mbinu za kinidhamu zisizo hatarishi.

Dawati la Jinsia na watoto jijini Dodoma limesema lipo tayari kumchukulia hatua kali za kisheria mzazi au mlezi atakae bainika kutoa adhabu ya kipigo kikali kwa mtoto.

Vipigo vilivyo pitiliza kwa watoto vinachukuliwa kama ukatili wa kimwili na ukiukaji wa haki za mtoto, ambao mara nyingi huathiri watoto kwa misingi ya kijinsia.

Dawati la jinsia huona kuwa ipo haja ya kuchukua hatua kali za kisheria kwa wazazi wanao tekeleza vitendo hivyo kama anavyo bainisha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto Christer Kayombo wakati akizungumza na Taswira ya Habari.

Sauti ya Christer Kayombo.

Je, ni sababu gani hasa huwafanya wazazi au walezi kutumia adhabu ya vipigo vikali kwa watoto? Na hapa Mrakibu anaeleza zaidi.

Sauti ya Christer Kayombo.

Aidha amewataka wazazi na walezi kutumia njia mbadala za adhabu, zinazo msaidia mtoto kuelewa makosa yake na kujirekebisha, bila ya kumuumiza kimwili au kisaikolojia. Njia hizi hutoa nafasi kwa mtoto kujifunza maadili mema.

Sauti ya Christer Kayombo.