Dodoma FM

Ramli chonganishi yapelekea mwanafunzi kupoteza maisha

18 August 2025, 5:51 pm

Hadi sasa, wanafunzi 11 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika katika tukio.Picha na Kitana Hamis.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limefika katika eneo la tukio na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.

Na Kitana Hamis.
Mtoto Yohana Amani Konki (17), mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Qashi, wilayani Babati Mkoani Manyara, amepoteza maisha kwa tuhuma za wizi wa simu baada ya kushambuliwa na wanafunzi wenzake kufuatia madai ya ramli chonganishi iliyotolewa na mganga wa kienyeji.

Tukio hilo limetokea Aug.16, 2025 katika kata ya Qashi ambapo inadaiwa kuwa mganga huyo alimtaja marehemu kupitia ramli kuwa ndiye aliyehusika na wizi wa simu, jambo lililowachochea wenzake kumvamia na kumsababishia majeraha yaliyosababisha kifo chake.

Picha ni baadhi ya wazazi wakiwa shuleni hapo baada ya tukio hilo kutokea.Picha na Kitana Hamis.

Hadi sasa, wanafunzi 11 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo la mauaji.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa hatua hiyo ya kujichukulia sheria mikononi ilitokana na imani potofu badala ya uthibitisho wa kisheria.

Habari kamili.