Dodoma FM

Wagombea waendelea kujitokeza kuchukua fomu

18 August 2025, 3:09 pm

Picha ni Mkurugenzi wa INEC, Ndugu, Kailima Ramadhani .Picha na INEC.

Ikumbukwe kuwa Zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi wa kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 limeanza rasmi tarehe 14 Agosti 2025 na linatarajiwa kumalizika tarehe 27 Agosti 2025, kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Na Lilian Leopold.
Wakati zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa Ubunge na Udiwani likiendelea,Wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa wameendelea kujitokeza kuchukua fomu hizo katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi.

Hali imekuwa hivyo kwenye Jimbo la Mtumba na Dodoma mjini ambapo Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba, Wakili Cosmas Nsemwa akizungumza na waandishi wa habari amesema mpaka sasa ni wagombea 11 waliochukua fomu ya kugombea.

Katika zoezi hilo la baadhi ya wagombea wameonesha dhamira ya kuwatumikia wananchi kama wanavyoeleza.

Habari kamili.