Dodoma FM

NGO’s zatakiwa kuwajibika katika kuwahudumia wananchi

12 August 2025, 11:27 am

Picha ni washiriki katika Kongamano la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.Picha na Maendeleo ya jamii.

Naibu Waziri Mwanaidi ameeleza kwamba uwazi na uwajibikaji wa Mashirika hayo ndiyo msingi wa kutambuliwa kwa mchango wao katika maendelo ya Taifa.

Na Mariam Matundu.
Mashirika yasiyo ya Kiserikali yametakiwa kuwa wazi na kuwajabika katika utekelezaji wa majukumu yao hasa kuwahudumia wananchi .

Hayo yamesemwa Agosti 11, 2025 na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis wakati akifungua Kongamano la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Picha ni washiriki katika Kongamano la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.Picha na Maendeleo ya jamii.

Aidha amesisitiza kwamba kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanapaswa kutoa elimu ya kiraia kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu ili kutimiza haki yao ya kidemokrasia.

Sauti ya Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amesema Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni nyenzo muhimu katika kutoa huduma kwa wananchi, hivyo ameyaasa Mashirika hayo kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendeleo kuhakikisha wananchi wananufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Sauti ya Wakili Amon Mpanju

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mwantum Mahiza amesema Bodi hiyo inaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha NGOs zinafuata kanuni na taratibu zilizopo ili kufanikisha maono yao katika kuwahudumia wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Gasper Makala asema Baraza hilo limeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Mashirika hayo yanashirikiana na Serikali na wadau wengine katika kuwahudumia wananchi kupitia utekelezaji wa miradi.