Dodoma FM

Dosari karatasi za kupigia kura zakwamisha uchaguzi

5 August 2025, 5:45 pm

Katibu Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja akitolea ufafanuzi .Picha na Kitana Hamis.

Amesema hitilafu katika uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura kwa baadhi ya majina ya wagombea kukosewa na kutoonekana imesababisha zoezi hilo kutofanyika.

Na Kitana Hamis.
Katibu Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja ametolea ufafanuzi sababu za kata mbili ya Mikese na Tindiga kushindwa kufanyika Uchaguzi kura za maoni za udiwani na Ubunge.

Amefafanua kuwa kwa Kata ya Tindiga Jimbo la Mikumi zitapigwa kura za nafasi ya udiwani na ubunge, na kwa kata ya Mikese Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki zikipigwa za nafasi ya udiwani pekee na kwamba uchaguzi katika maeneo hayo utafanyika Leo Agosti 5 mwaka huu.

Sauti ya Nuru Ngereja.