Dodoma FM

Nafasi ya watu wa karibu kumuepusha mwanaume na changamoto ya afya ya akili

30 July 2025, 1:53 pm

Changamoto ya afya ya akili kwa wanaume ni kubwa kuliko kwa wanawake.Picha na Afya ya akili.

Aina ya malezi wanayopitia baadhi ya wanaume wakati wa utoto wao yanaweza kuwa sababu ya changamoto ya afya ya akili.

Na Seleman Kodima.
Imeelezwa kuwa aina ya malezi wanayopitia baadhi ya wanaume wakati wa utoto wao yanaweza kuwa sababu ya changamoto ya afya ya akili kwao kwa siku za baadae.

Awali nilizungumza na mtaalamu wa saikolojia Peter Njau ambao ameeleza kuwa changamoto ya afya ya akili kwa wanaume ni kubwa kuliko kwa wanawake ambapo sababu ya malezi ni chanzo kikuu cha matatizo hayo.