Dodoma FM
Dodoma FM
30 July 2025, 12:57 pm

Ikumbukwe kuwa Ripoti za uwajibikaji zinazotolewa na taasisi ya Wajibu huangazia hoja kuu zilizobainishwa na CAG, kama matumizi mabaya ya fedha, miradi iliyotelekezwa, au taasisi zilizopata hati mbaya3.Hii husaidia wananchi kuelewa maeneo yenye changamoto na kuhoji uwajibikaji wa viongozi wa umma.
Na Seleman Kodima.
Katika kufanikisha wananchi kwa Ujumla wanafutailia Ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali CAG,Taasisi ya Wajibu Tanzania kwa kushirikiana na Policy Forum kwa mara ya kwanza wamezindua ripoti ya uwajibakiji yenye nukta nundu sambamba na Ripoti za kawaida zenye lengo la kuwapa uelewa wananchi katika muktadha wa ripoti ya CAG.
Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma na kuhudhuri na wadau mbalimbali kutoka taasisi zisio za kiserikali,Taasisi za umma,wadau wa maendeleo,waandishi wa habari na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali jijini hapa.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti,Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Wajibu Tanzania,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh amesema ripoti hizo ni muendelezo wa kuhakikisha wananchi wanafahamu ripoti ya CAG.
Semkae Kilonzo,ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Policy Forum amebainisha sababu za wao kuungana na Taasisi ya Wajibu katika ufanikishaji wa ripoti hizo tatu.