Dodoma FM

Mitazamo hasi inasababishaje changamoto ya afya ya akili?

22 July 2025, 1:08 pm

Zipo sababu tofauti ikiwemo matukio ya kujiua yaliongezeka kutoka 35 mwaka 2022 hadi 57 mwaka 20232. Picha na Google.

Kutokana na hali hiyo, mapema Seleman Kodima alifanya mahojiano na Apolioni Boniphace kutoka Taasisi ya Whole Health Junction na hapa anaeleza zaidi.

Na Seleman Kodima.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambayo ilichambua hali ya afya ya akili nchini, imebainisha kuwa wagonjwa wa afya ya akili waliongezeka kutoka 386,358 mwaka 2012 hadi 2,102,726 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 82.

Aidha Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2023, iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ilibainisha kuwa zipo sababu tofauti ikiwemo matukio ya kujiua yaliyoongezeka kutoka 35 mwaka 2022 hadi 57 mwaka 20232. Wanaume walihusika katika asilimia 79 ya matukio hayo, ikilinganishwa na asilimia 83 mwaka uliopita.

Vijana wa miaka 15–35 walichangia asilimia 46 ya matukio ya kujiua, wakifuatiwa na watu wa makamo (36–59) kwa asilimia 27.