Dodoma FM
Dodoma FM
9 July 2025, 3:29 pm

Lengo kuu La mkopo wa asilimia 10 kutoka halmashauri ni kuwezesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi kwakuwapatia mkopo wenye masharti nafuu ili kupunguza umaskini na kukuza ajira.
Na Lilian Leopold.
Wananchi kata ya Mpunguzi jijini Dodoma wametakiwa kujitokeza kuchangamkia fursa ya mkopo wa asilimia 10 ili kujikwamua kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Afisa Maendeleo Kata ya Mpunguzi Frank Mgongolwa wakati akizungumza na Taswiraya Habari, ambapo ameongeza kuwa jumla ya vikundi 18 tayari vimejisajiri katika mfumo wa Wezeshapoto.
Aidha amesemajumlaya shilingi milioni 78 na laki 2 zimetolewa kwaajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Victoria Elieza ni mnufaika wa mkopo wa asilimia 10 amesema mkopo huo umekua mkombozi kwake na wanakikundi kwani waliutumia kuanzisha kilimo.