Dodoma FM
Dodoma FM
16 April 2025, 5:42 pm

CAG Kichere amesema kuwa ripoti ya ukaguzi za mwaka 2023/2024 tayari zimewasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na zinapatikana katika tovuti ya ofisi ya ukaguzi kuruhusu wananchi na wadau kupitiaripoti hiyo.
Na Yussuph Hassan.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere ameshauri Bunge kujadili ripoti za ukaguzi pindi zinapotoka tu badala ya kusubiri baada ya muda fulani.
Wito huo umeutoa leo Jijini Dodoma katika mkutano wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na waandishi wa habari na viongozi wengine juu ripoti za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka 2023/ 2024.
Bw Kichere amesema licha kuwepo mabadiliko makubwa kwa sasa ila bado wanaendelea kushauri bunge kuangalia utaratibu wa kuzijadili ripoti hizo mapema.
Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya LAAC Mhe Halima Mdee amesema kwenye baadhi miradi ya maendeleo hakuna thamani ya fedha huku akipongeza ofisi ya CAG kuendelea kuboresha eneo hilo.
Naye Makamu mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji wa mitaji ya umma CPA Marry Masanja amesema ni muhimu kwa mashirika kufanyia katika ripoti za CAG ili kuboresha katika maeneo yao.
Itakumbukwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Edward Kichere tarehe 27 Machi, 2022 aliwasilisha ripoti yake Ikulu, Dar es Salaam mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, Kichere amebainisha kuwa kuhusu kaguzi maalumu na kaguzi za kiuchunguzi 52 ambazo ofisi ya CAG imefanya, 44 zilitokana na maombi ya wadau mbalimbali na kaguzi nane ziliibuliwa na ofisi yake kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa ya kikatiba na kisheria.