Dodoma FM

Ajinyonga hadi kufa kisa msongo wa mawazo

15 April 2025, 3:51 pm

Picha ni mwili wananchi wakiwa wamebeba mwili wa mtu huyo aliye jinyonga.Picha na Kitana Hamis.

Asubuhi alikwenda shambani kuandaa mkaa aliporudi nyumbani alipewa uji na mke wake anywe na baadaye alirudi tena shambani ambapo alikutwa amejinyonga .

Na Kitana Hamis.
Mtu Mmoja aliyefamika kwa Jina la Jumanne Idi Mkazi wa Kata ya Sigino Kijiji cha Imbilili Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara amedaiwa kujinyonga chanzo kikidaiwa kuwa nimsongo wa Mawazo .

Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wananchi ambao walishuhudia tukio hili wakati Mwili wamarehemu Jumanne idi ukiondoshwa katika eneo la tukio wanasema chanzo Cha kifo chake bado hakijajulikana .

Dodoma fm imezungumza na Mke wa marehemu ambapo anasema asubuhi alikwenda shambani kuandaa Mkaa aliporudi Nyumbani alipewa Uji na mke wake anywe na baadae alirudi tena shambani ambapo alikutwa amejinyonga .

Sauti ya Kitana Hamis