

14 April 2025, 5:36 pm
Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi amewataka wananchi kuacha tabia ya kupokea mali za wizi na iwapo watangundua tukio lolote la uhalifu watoe taarifa katika mamlaka husika.
Na Lilian Leopord.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi amesema kuwa matukio ya wizi wa mali ikiwemo simu umeendelea kukua katika Jiji la Dodoma.
Katabazi ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati alipokutana na wauzaji na mafundi wa simu na tv zilizotumika lengo ikiwa ni kubaini na kutatua changamoto za uhalifu.
Aidha Katabazi amebainisha maazimio waliyoyaweka katika kukabiliana na uhalifu ikiwemo kuendeleza ushirikiano na kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Masuala ya Wateja na Watumiaji ya Mamlaka ya Hali ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA) Kadaya Balugye, amesema kutokana na takwimu zilizokuwa zikitolewa na TCRA kuanzia mwezi Juni majaribio ya ulaghai wa mtandao katika Mkoa wa Dodoma unaendelea kupungua.
Baadhi ya wauza simu na mafundi simu waliojitokeza katika kikao hicho wamesema kuwa kutokana elimu waliyoipata itawasaidia sana na kupunguza idadi ya uhalifu.