

2 April 2025, 6:00 pm
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, asilimia 11.2 ya watu wote nchini wana ulemavu, idadi hiyo imeongezeka kutoka asilimia 9.3 ilivyokuwa katika sensa ya mwaka 2012.
Na Lilian Leopord.
Katika jamii, lugha ina nguvu kubwa katika kuunda mitazamo na hisia kuhusu makundi mbalimbali ya watu. Hata hivyo, matumizi ya majina na lugha zisizofaa, yanaweza kuathiri vibaya jinsi tunavyowatendea wengine, hasa wale wenye ulemavu.
Sheria za kuwalinda watu wenye ulemavu, ikiwemo watu wenye ualbino na wasioona ni muhimu sana katika kuhakikisha haki zao zinaheshimiwa na wanapata fursa sawa katika jamii.
Mwamrisho Kasule ni Afisa kutoka Taasisi ya Foundation for Disablities Hope, taasisi inayohusika na kutetea haki za watu wenye ulemavu jijini Dodoma, amebainisha sheria zinazohusika kuwalinda watu hawa.
Aidha, Mwamrisho ameongeza kuwa mtu anapoitwa kwa jina ambalo linaonyesha udhaifu au kasoro inaweza kuathiri jinsi wanavyojiona wao wenyewe.
Kwa upande wake Irene Julias ambaye ni mmoja wa wafanyakazi katika taasisi hiyo ameelezea mikakati tofauti wanayoitumia ili kubadili mtazamo wa jamii kuhusu majina yasiyofaa.
Wananchi Jijini Dodoma, wameonesha hisia tofauti kuhusu tabia ya baadhi ya watu kuwaita watu wenye ulemavu majina yasiyofaa.