

11 March 2025, 11:07 am
Hata Hivyo dhamana ya watuhumiwa hao ipo wazi lakini washitakiwa walishidwa Mashariti ambayo yalihitaji kila Mtuhumiwa adhaminiwe na Watu wawili ambao niwatumishi wa Serikali nawawe na sh: Milioni Tano.
Na Kitana Hamis.
Watumishi Watatu wa Serikali za Vijiji Engusero wapandishwa Kizimbani Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Walio fikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto ni Robati Mchambui Mwenyekiti wa wa Kijiji cha Engusero Wilayani Kiteto, Mwachiwa Mgome Huyu nimwenyekiti wa Kitongoji Cha Engusero na Jorome maiko Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Mabululu Kwamujibu wa Mwendesha Mashtaka Yahaya Masaa kilija Katikati Mahakama ya Wilaya ya Kiteto anasema washitakiwa hao niwatumishi wa Serikali ambao wanashitakiwa kwa makosa nane (8).
Shtaka la Kwanza hadi Shtaka la Saba (7) nimatumizi mabaya ya Madaraka Shtaka Moja ni la Uhujumu Uchumi amesema Watuhumiwa wametenda Kosa Kinyume na Kifugo Cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kama ilivyo fanyiwa mapitio mwaka 2022.
Maelezo ya kosa nikwamba Watumiwa hao Waliuza Ardhi ya Kijiji Ekari 10.5 kwakikiuka Kifungu Cha Sheria namba 8 Kifungu kidogo Cha namba 5 cha Sheria ya Ardhi ya Kijiji Sura ya 114 Kama ilivyo fanyiwa marejeo Mwaka 2019.
Mwendesha Mashtaka Masaa kilija Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wamahakama Ya Wilaya ya Kiteto Boniface Lihamwike amesema watuhumiwa hao kwanyakati Tofauti walitenda Makosa 8 kwa Makusudi wakiwa katika maeneo yao ya Kijiji cha Engusero.
Akisoma kosa la 8 ambalo ni ubadhilifu wa Fedha kiasi cha sh: Milioni mbili na laki sita ambazo zilipatika kwa kuuzwa kwa Aridhi hio ya Kijiji Kinyume cha Sheria.Anasema kosa la 8 niubadilifu wa Fedha kiasi cha Zaidi ya Sh: Milioni mbili na laki sita ambazo zilipatika kwa kuuzwa kwa Aridhi ya Kijiji Kinyume cha Sheria.