

6 March 2025, 5:34 pm
Miaka kadhaa iliyo pita alimpoteza Mume wake Hali ya maisha yake ilibadilika na kupelekea yeye na familia yake kukosa mahali pa kuishi.
Na Kitana Hamis.
Jeshi la Polisi Wilayani Babati Mkoani Manyara limemfariji Mjane Mwenye Watoto Sita kwa kumkabidhi kiwanja na Fedha.
Leah Isaac nimama Mjane mwenye Watoto Sita ambaye miaka kadhaa iliyo pita alimpoteza Mume wake Hali ya maisha yake ilibadilika na kupelekea yeye na familia yake kukosa mahali pa kuishi.
Wanawake wa Jeshi la Polisi Pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Manyara vimemtembelea mama huyo na kumkabidhi kiwanja ili aweze kujenga makazi yake ya Kudumu.
Ernesta Mwambinga nikaimu Mwenyekiti wa TPF Net Mkoa wa Manyara ambaye pia nimkuu wa Polisi Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Nahapa anaeleza namna Jeshi hilo lilivyo nguswa na Maisha ya mama huyu.