

25 February 2025, 6:26 pm
Hata hivyo Jeshi hilo linaomba rai kwa Wananchi walio tapeliwa kufika ili kuweza kutambua simu zao zilizo ibiwa.
Na Kitana Hamis.
Jeshi la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia Mtu Mmoja aliye julikana kwa Jina la Victor Onesmo Mwenyewe umri wa Miaka Thelathini ( 30 ) kwa Tuhuma za kujifanya Daktari na kuwalaghai Wanawake Kingono na kuwapeleka Nyumba za Kulala Wageni na baadae kuwaibia Vitu Vyao ikiwemo Simu na Fedha.
Akizungumza na Wandishi wa Habari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara SACP Ahmed Makarani. Anasema katika Tukio hilo la ulaghai wa Kingono Kijana alie kamatwa na Jeshi hilo ni Victor Onesmo Marufu kama (BAMTU) katika Mtandao wa Tiktock ambapo Mtuhumiwa amekuwa akijifanya Daktari kisha kuwalaghai Wanawake Kingono Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi hilo huku akiwa na kielelezo cha simu janja Kumi na Saba ( 17)
.