

12 February 2025, 3:36 pm
Siku ya usalama mtandaoni duniani huadhimishwa Jumanne ya pili ya mwezi Februari kila mwaka ambapo ni mpango wa kimataifa ulionzishwa mwaka 2004.
Na Seleman Kodima.
Imeelezwa kuwa Usalama wa mtandaoni ukiimarishwa utasaidia kujenga imani kwa watumiaji wengi na kupanua wigo wa utumiaji wa mtandao hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Dkt Jones Killimbe katika maadhimisho ya siku ya usalama mtandaoni 2025 yalioyafanyika jijini Dodoma.
Awali Mwakilishi wa mkurugnezi mkuu wa TCRA ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Leseni na ufuatiliaji Bw John Daffa ametaja sababu zinazopelekea watumiaji wa mtandao kuchangia matukio yanayohatarisha usalama mtandaoni.
Aidha katika maadhimisho hayo yamewakutunisha wadau mbalimbali ikiwemo wanafunzi kutoka Vyuo ,Shule za Sekondari ambapo baadhi ya washiriki kutoka taasisi hizo wameelezea namna wanavyojilinda na hatari mtandaoni.
Siku ya usalama mtandaoni duniani huadhimishwa jumanne ya pili ya mwezi Februari kila mwaka ambapo ni mpango wa kimataifa ulionzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kuhamasisha matumizi sahihi na salam ya mtandao wa internet.