Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuona fursa kwenye uchumi wa kidigitali

7 February 2025, 3:58 pm

Picha ni Mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi na washindi katika hafla ya shindano la sita la Masuala ya Usalama Mtandaoni’cyberchmapions 2025 lililofanyika katika Chuo kikuu cha Dodoma UDOM.Picha na Seleman Kodima.

Ikumbukwe kuwa Shindano hili la Masuala ya Usalama Mtandaoni’ yaan CyberChampions 2025 linaratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuibua, kuimarisha na kukuza uwezo kwa vijana kukabili vihatarishi vya usalama mtandaoni na kushiriki kikamilifu kwenye uchumi wa kidijiti.

Na Seleman Kodima.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari amesema ni muhimu kuweka jitihada katika kuwandaa watu kwa kuwapa maarifa na ujuzi ili kwenda sambamba na mfumo wa uchumi wa kidijiti.

Wito huo umeutoa Wakati Halfa ya shindano la sita la Masuala ya Usalama Mtandaoni’cyberchmapions 2025 lililofanyika katika Chuo kikuu cha Dodoma UDOM.

Sauti ya Dkt. Jabiri Bakari .

Akitoa Msisitizo kwa washiriki wa shindano hilo ambao ni wanafunzi kutoka kwenye vyuo mbalimbali hapa nchini ,Mkurugenzi wa TCRA hapa nchini Dkt Jabiri amesema ni muhimu kuwe maandalizi ya kutosha ili kupata watu wenye kufanikisha uchumi wa kidijiti.

Picha ni Mgeni rasmi katika hafla hiyo akiwa katika picha ya pamoja na moja ya washindi wa washindano hilo.Picha na Seleman Kodima.
Sauti ya Dkt. Jabiri Bakari .

Baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba amewapa pongezi wote waliofanikiwa kushinda na kutoa nafasi ya internship kwenye kituo hicho wakati wowote baada ya masomo yao hii ikiwa sehemu ya zawadi kwa washindi wa mwaka huu.

Aidha kituo hiki kimezungumza na Kaimu Rasi wa ndaki wa Compture ya sayansi na Elimu Angavu Dkt Florence Rashid ambapo Wanafunzi wa Chuo hicho wameibuka washindi katika shindano hilo la Usalama mtandaoni na kubainisha namna walivyopokea ushindi huo.

Sauti ya Dkt Florence Rashid .

Meshack Edward ni Mwanfunzi wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa kuendelea kufanya mashindano hayo yenye lengo la kuongeza hamasa kwa wabunifu na kukuza uwezo wa vijana katika suala la usalama mtandaoni.
Clip 4 Meshack.