

3 February 2025, 11:57 am
walifanikiwa kuwakamata wahalifu huku wakiwa na ushahidi lakini walikumbana na vitisho dhidi ya oparesheni hiyo.
Na Kitana Hamis.
Vita thidi ya Dawa za Kulevya Mirungi na Bangi hapa Wilayani Kiteto Mkoani Manyara inatajwa kuwa na Changamoto Kubwa na inaelezwa kuwa kila Kukicha wahalifu wanakamatwa na Kuachiwa .
Wananchi wa Kijiji cha Njoro Wilaya Kiteto Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara wanasema wakiwa Kwenye Operesheni ya Kupambana na kuzuia dawa za Kulevya Kwenye Kijiji yasiuzwe walifanikiwa kuwakamata wahalifu huku wakiwa na ushahidi lakini walikumbana na vitisho dhidi ya oparesheni hiyo.
Afisa Mtedaji wa kata anatajwa kuwa nimiongoni mwa watu wanao kwamisha zoezi hilo .
Katika Mkutano huo kukawa na Maswali na Majibu kati ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara na afisa huyo Mtedaji wa kata ambapo baada ya mahojiano Mh Queen Sendiga alitoa maamuzi .
Swaala la Mgogoro wa Aridhi nalo likaibuka kwawananchi hao kuonesha jinsi migogoro inavyo waathiri katika wilaya hiyo.