Kituo cha wasioona Buigiri chaiomba serikali na wadau kuwakumbuka katika kilimo
11 December 2024, 5:28 pm
Wanaeleza kuwa tangu kujengwa kwa kituo hicho zaidi ya miaka 30 hakuna msaada wa kujitosheleza unaotolewa na Serikali katika kituo hicho licha ya jamii yake kujikita katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji.
Na Victor Chigwada.
Wakulima wa bustani za mbogamboga kutoka kituo cha wasio ona Buigiri wameiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo kuwasadia ruzuku za kilimo ikiwa na pamoja na samadi za kukuzia mimea.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kilimo katika kituo hicho Ndg.Meshaki Mosesi kwani wameshindwa kumudu gharama za kununua mbolea kwaajili ya bustani zao.
Mosesi amesema kuwa ktuo chao kinategemea kilimo hicho kuendesha maisha ya familia zao lakini changamoto ya kukosa dawa za kuuwa wadudu pamoja na mbolea imekuwa kikwazo cha kukuza mitaji yao.
Aidha ameongeza kuwa licha ya kuwa ni msimu wa mvua kwasasa lakini wanakumbanma na adha ya maji ya kumwagilia mboga zao katika kipindi cha kiangazi.
Changamoto hiyo imekuwa ikichagizwa na kuishiwa Luku ya umemne hivyo ni vyema Serikali kuwawekea mfumo mbadala wa umeme jua kusadia nyakati ambazo wameishiwa Luku.
Nao baadhi ya wakazi wa kambi hiyo wamekiri kukabiliwa na changamoto hizo upande wa kilkimo nakuomba mamlaka husika kuchukua hatua za kutatua kwani ndiyo sehemu yao ya maisha.
Inaelezwa hali ya kituo hicho cha makazi ya watu wasioona Buigiri ni kama kimetengwa na wala Serikali haikioni hali inayowafanya walemavu hao wajiulize maswali kama Serikali inakitambua au hakitambui