Fahamu faida za hifadhi hai za Tanzania
5 November 2024, 5:58 pm
Na Fred Cheti.
Nevomba 3 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya hifadhi hai duniani ambapo kuna hifadhi hai zipatazo 748 huku Tanzania ikiwa na jumla ya hifadhi hai 6.
Bwn. Novatusi Moshi ni Afisa Mazingira mwandamizi kutoka Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC anaelezea umuhimu wa kulinda hifadhi hai zilizopo.
Aidha Bwana Mushi anasema kuwa mbali na hifadhi hai hizo kusaidia katika kuboresha mazingira pia zimekuwa na faida kubwa za kiuchumia endapo zitalindwa vizuri
Baraza la Taifa la uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira limetoa wito kwa jamii kuhifadhi na kulinda hifadhi hai zilizopo nchini ili kuzidi kuboresha mahusiano ya binadamu,ekolojia na Mazingira.