Watatu wanusurika ajali ya moto bajaj ikiteketea
29 October 2024, 3:59 pm
Na Anwary Shabani
Watu watatu jijini Dodoma wamenusurika kifo baada ya bajaji waliyokuwa wakiitumia kwa safari za mjini kuwaka moto na kuteketea katika mtaa wa Kitenge Kata ya majengo.
Bwn Isaack Gideon ambaye ni dereva wa bajaj hiyo anaeleza jitihada alizozichukua kwa kusaidiana na wananchi ili kukabiliana na moto huo.
Aidha mashuhuda wa ajali hiyo wametoa maoni yao ili kuepuka matukio kama hayo hasa kwa vyombo vya usafiri,
Ili kuepuka ajali za moto katika vyombo vya usafiri inashiriwa kufanyika kwa ukaguzi wa chombo cha usafiri ili kubaini mambo yanayoweza kusababisha ajaili ya moto kama vile kuvuja kwa mafuta, itilafu katika mfumo wa breki pamoja na matengenezo duni. Ajali hiyo ya moto imetokea Oktoba 28, 2024.