Betri chakavu za magari ni hatari kwa afya
23 October 2024, 12:55 am
Na Mariam Kasawa.
Taka za betri chakavu zinatajwa kuwa na athari kimazingira na kiafya kwa binadamu hivyo umakini unahitajila katika kuziteketeza au kurejelezwa.
Akizingumza katika wiki ya kujiondosha na kuepukana na taka za As lead zinazotokana na betri chakavu, Bwn . Hamad Taimuru Meneja Uzingatiaji Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC amesema viwanda vyote vinatakiwa kufanya tathini ya athari kwa mazingira ili kujua miiko iliyowekwa ya urejelezaji wa taka.
Aidha amesema wamekutana na wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki wa viwanda ili waweze kuona urejezeji wa betri chakavu unavyo fanyika katika viwanda.
Taka za betri chakavu zinatajwa kuwa na athari kimazingira na kiafya kwa binadamu hivyo zinapaswa kuteketezwa au kurejelezwa ili zisilete athari katika mazingira.