Dodoma FM

NIMR  yatafiti mikakati ya chanjo ya Uviko-19

18 October 2024, 8:05 pm

Na Yussuph Hassan.

Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii ESRF kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR zimefanya utafiti wa kutathmini mikakati ya kuongeza upataji chanjo ya Uviko-19 nchini.

Akizungumza jijini Dodoma katika kongamano la sera ya Taifa la kutoa matokeo ya utafiti huo lililowaleta pamoja wadau wa chanjo, mkuu wa utawala na maendeleo ya uwezo kutoka ESRF Bw.Danford Sango anaeleza sababu za kufanya utafiki huo. Kongamano hilo lilifanyika Oct. 16, 2024.

Mkuu wa utawala na maendeleo ya uwezo kutoka ESRF Bw. Danford Sango
Sauti ya Bwn. Danford Sango

Bwn. Andrew Kilale ambaye ni afisa mkuu wa tafiti kutoka NIMR  anaeleza jinsi chanjo ya Uviko-19  ilivyokabiliwa na changamoto nyingi baada ya baadhi ya makundi mbalimbali kuipinga.

Pichani afisa mkuu wa tafiti kutoka NIMR  Bwn. Andrew Kilale
 Sauti ya Bwn. Andrew Kilale

Aidha Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya Bwn. Victor Kweka  anaeleza matarajio yao baada ya kufanyika kongamano hilo.

Pichani Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya Bwn. Victor Kweka
Sauti ya Bwn. Victor Kweka

Utafiti huo ulihusisha kampeni ya kutuma jumbe fupi kwa kundi la jamii lililochaguliwa kuhusu athari za uviko-19 kuona kama inaweza kuhimiza watu kuchanja ambapo lengo lilikuwa kufikia watu elfu 12 kwa sms ambapo awamu ya kwanza walifikia watu elfu nane na ya pili elfu 3.