Dodoma FM

NEMC yaagiza viwanda kufanya tathmini ya mazingira kabla Octoba 30

9 October 2024, 6:22 pm

Na Mariam Kasawa.

Balaza la Uhifadhi na Usimaizi wa Mazngira NEMC limetoa mwezi mmoja kwa  viwanda kufanya tathmini za athari kwa mazingira ili kuepuka uchafuzi wa mazingira unaosababisha na shughuli za viwanda.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi ambapo amewataka wenye viwanda  kutimiza agizo hilo kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria ifikapo tarehe 30 ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi
Sauti ya Dkt. Immaculate Sware Semesi

Itakumbukwa kuwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa oktoba 5,2024 akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Temeke alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NEMC kutembelea viwanda vya Mbagala vinavyotiririsha maji kwenye makazi ya watu.

Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa
Sauti ya Mh. Kassim Majaliwa

Pia NEMC imevitaka viwanda vya uzalishaji wa aina yoyote nchini kufanya tathmini ya athari kwa mazingira na viwanda vyenye vyeti vizingatie matakwa ya vyeti hivyo vya mazingira.