Dodoma FM

Madiwani Dodoma wahimiza uandikishaji daftari la kupiga kura

24 September 2024, 8:31 pm

Na Fredi Cheti.

Wananchi jijini Dodoma wametakiwa kujiandikisha pamoja kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Mpiga kura ili wapate haki yao ya Msingi na ya kikatiba ya kuchagua viongozi.

Zoezi la uandikishaji katika daftari la kupiga kura katika Halmashauri ya jiji la Dodoma linatarajia kuanza 25 Septemba 2024 katika kata mbalimbali ikiwemo kata ya Msalato kama ambavyo anabainisha Afisa uandikishaji kutoka kata ya Msalato Devotha John.

Afisa uandikishaji kata ya Msalato Bi. Devotha John
Sauti ya Bi. Devotha John

Baadhi ya Madiwani katika halmshauri ya jiji la Dodoma wamekuwa wakitoa  hamasa  kupita vyombo vya habari kwa wakazi wa Dodoma ili kushiriki kwenye chaguzi zijazo ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mtaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani.

Bwn. Edward Magawa Diwani wa Kata ya Ihumwa
Sauti ya Bw, Edward Magawa na Bi. Paskazia Myala
Bi. Paskazia Myala Diwani wa kata ya Mbabala

Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa   27 Novemba 2024 pamoja na uchaguzi mkuu mwakani . Wananchi wanahimizwa kujiandisha pamoja na kuboresha taarifa zao ili waweze kushirika katika chaguzi hizo.